Sunday, January 29, 2012

TWIGA STARS YA NG'ARA UWANJA WA TAIFA

Team ya taifa ya wanawake Twiga stars 'the dream team' imeonyesha umahiri mkubwa katika kulisakata soka hapa nchini na kuiperusha bendera ya taifa juu kabisa baada ya kuifunga timu ya taifa ya Namibia mabao 5 kwa 2. Meneja wa kikosi hicho Kocha mzoefu Charles Bonifas Mkwasa jana alipokea sifa kem kem baada ya kikosi chake kuonyesha umahiri mkubwa  hasa nyota wa mchezo huo Mwanahamisi Omari.

Dream Coach Charles Bonifas Mkwasa
Mwanahamisi Omari akihojiwa
Twiga walionekana kutawala sana mchezo huo. Licha ya Namibia kusawazisha mabao mawili ya kwanza, lakini walipoteana katika dakika za mwisho na kuwapa mwanya kinadada wa Kitanzania kuonyesha makeke yao na kufanikiwa kupata mabao matatu katika dakika 10 za mwisho.

Washabiki wakiwa katika nyuso za furaha.

Mbali na ushindi huo timu hiyo ilikabidhiwa shilingi milioni nne kutoka kwa Waziri wa Habari, Utamaduni na michezo, Dk Emmanuel Nchimbi pamoja na wabunge walioahidi kutoa shilingi milioni moja ikiwa timu hiyo itashinda.
Katika mchezo huo, mabao ya  Namibia yalifungwa na Juliana Skrywer, pamoja na bao moja la zawadi baada ya beki Fatma Bashir kujifunga.
 Mwanahamisi Omari akipongezwa na wenzie

 Twiga walionekana kutawala sana mchezo huo. Licha ya Namibia kusawazisha mabao mawili ya kwanza, lakini walipoteana katika dakika za mwisho na kuwapa mwanya kinadada wa Kitanzania kuonyesha makeke yao na kufanikiwa kupata mabao matatu katika dakika 10 za mwisho.
Baada ya mechi hiyo, Twiga walipata wakati mgumu walipotaka kuondoka uwanjani baada ya mashabiki kulizingira gari lao huku wakishangilia na kuimba kwa furaha, polisi waliingilia na kutoa msaada.
Baada ya ushindi huo, Twiga itacheza na Misri au Ethiopia katika hatua inayofuata na kocha wa timu hiyo, Boniface Mkwasa, ametamba kuendeleza ushindi.






No comments:

Post a Comment

wadau unakaribishiwa kutoa comment ilimradi ziwe za kujenga na kuelimisha pia