Friday, April 29, 2011

HARUSI YA PRINCE WILLIAM NA VITUKO VYA KILA NAMNA

GORDON BROWN ,TONNY BLAIR WAKOSA MUHALIKO,BALOZI WA SYRIA NA MALAWI MIHALIKO YAO YAFUTWA GHAFLA  


Harusi ya mjukuu wa Malkia Elizabeth wa uingereza inayotaraji kufungwa masaa machache yajayo imeambatana na vituko mbalimbali na vya kustahajabisha baada ya mawaziri wakuu Tony Blair na Gordon Brown kunyimwa muhaliko huo muhimu kilichopelekea watu hawa kukosa muhaliko ni kile kinachodaiwa watu hawa ni wale wanaopinga utawala wa kifalme nchini humo kuwa hauna mana yoyote ktk dunia ya sasa,kwahiyo hawa mawaziri ni maadui wakubwa wa mda mrefu na koo hii ya kifalme,
Upande mwingine balozi wa Syria amefutiwa muhaliko wake baada ya vyombo vya habari kuandika habari nyingi kuwa balozi huyo wa Syria awezi kuhudhuria sherehe hizo ikiwa nchini kwake kuna matatizo bado,nae balozi wa Malawi kafukuzwa nchini humo baada ya balozi wa Uingereza nchini  Malawi kufukuzwa nchini Malawi kwa madai kuwa balozi huyo anamshutumu raisi wa nchi  hiyo bwana Joseph Chisano kuwa ni dikteta.na wako wengi muhimu waliokosa muhaliko huo basi hivi ni vituko vya kustahajabisha ndani ya harusi hii ya mjukuu wa malkia Elizabeth

    
 
GORDON BROWN



TONY BLAIR



Malawian ambasador


Prince William na Keth

No comments:

Post a Comment

wadau unakaribishiwa kutoa comment ilimradi ziwe za kujenga na kuelimisha pia