Tuesday, July 24, 2012

Diamond na Wema warudiana

Inasemakana baada ya kula maraha mjini kigoma penzi la vijana wenye umaarufu mkubwa nchini kwa sasa, Nasibu Abdu Juma ‘Diamond’ na Wema Isaac Sepetu limeanza upya huku ikisadikiwa kwa umakini kabisa kwamba mbunge wa huko huko mjini K akihusika na urejesho huo ambao ulikuwa na mizozo mingi sana.

Diamond na Wema wakiwa Kigoma
 Baada ya mda mrefu kupita huku Diamond na Wema wakiwa maadui wakubwa wa kutupiana maneno, kutambiana na wapenzi wapya kama ilivyotokea kwa Diamond kutamba na Binti Kidoti yaani Jokate Mwegelo, na pia kufia hata kuto pokea mkwanja aliotunzwa na Wema stejini siku ya usiku wa Diamond, mambo haya yote sasa yamehesabiwa kuwa ya kale na tugange yajayo kama nyimbo zenye msemo huu maarufu wa kiswahili usemwavyo.

Mambo yote yalianza pale Diamond na Wema, waliponaswa kwenye Tamasha la Kigoma All Stars, lililoandaliwa na Zitto kisha kufanyika Julai 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Shukurani kwa Zitto, kwani kupitia tamasha hilo, Diamond na Wema, waliweza kudhihirisha kwa kila mtu kwamba uhusiano wao sasa umerejea upya kwa kuambatana kimahaba ndani ya Mkoa wa Kigoma.


 Watu wengi wakijua kwamba kuna uhasama mkubwa kati ya Wema na Diamond, Julai 17, mwaka huu, ilikuwa ni mshangao wa aina yake kwa waliokuwepo Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Kigoma, baada ya vijana hao kushuka wakiwa wameongozana.

Diamond akiwa amevaa shati jekundu na tai nyeusi, chini akiondokea suruali ya jeans rangi ya bluu iliyopaushwa kimodo, huku Wema akitokelezea kwa koti la rangi ya maziwa, ndani blauzi nyeusi, halafu wote wameyaficha macho yao kwa miwani nyeusi, waliwaka vilivyo ndani ya Ujiji, Kigoma.
Baada ya kuwasili Kigoma, Wema na Diamond walielekea Hoteli ya Tanganyika Beach (ipo ufukweni mwa Ziwa Tanganyika) ambako walipata pumziko walilohitaji kabla ya nyota huyo wa wimbo wa Mbagala, hajaelekea Uwanja wa Lake Tanganyika kwenye Tamasha la Kigoma All Stars a.k.a Leka Dutigite.

Wema na Mama Diamond.
 Minong’ono ilitawala kila kona ya Mkoa wa Kigoma kwamba Wema amekwenda kuwakilisha Leka Dutigite, hivyo wakataraji kumuona Uwanja wa Lake Tanganyika, akitoa sapoti yake kwenye tamasha hilo.

Wapo ambao waliacha shughuli zao kwa ajili ya kwenda kumuona Wema tu uwanjani lakini waliambulia patupu, kwani mrembo huyo hakuonekana kabisa.
Kutokana na hali hiyo, wale waliovumisha stori kwamba Wema amekwenda Kigoma a.k.a Lwama, walionekana wazushi wasiofaa kusikilizwa, bila kujua kwamba mtoto alijificha ndani ya Hoteli ya Lake Tanganyika Beach.


Ingawa habari sa kuthibitika zinasema hao wawili walikua pamoja muda wote hivyo kuashiri kwamba mapenzi yanaendelea, huku Diamond akionekana kuwa mbali na wasanii wenzake katika tamasha hilo na kutumia muda mwingi kuwa na Miss Tanzania huyu wa mwaka 2006 ambae ana kismati cha kuwa na wapaenzi wengi kama vile Diamond anavyopendwa. Kinacho baki ni kwamba tuwaombee mapenzi yao yazidi na wasikie tena kiwango cha kukasana ki-namna vile kama mwanzoni.

No comments:

Post a Comment

wadau unakaribishiwa kutoa comment ilimradi ziwe za kujenga na kuelimisha pia