KITENDO cha mastaa wa filamu kushindwa kwenda kumtembelea msanii mwenzao,
Elizabeth Michael ‘Lulu’, anayekabiliwa na kesi inayohusisha kifo cha
aliyekuwa mwigizaji, Steven Kanumba, katika gereza la Segerea jijini Dar
ni kukwepa kuhusishwa katika keshi hiyo, imefahamika.
Uchunguzi
uliofanywa umebaini kuwa kumekuwa na mahudhurio hafifu ya
wasanii maarufu kwenda kumtembelea Lulu katika gereza hilo.
Akielezea
hali hiyo, kiongozi mmoja wa Bongo Movie, alisema ni kweli hali hiyo
ipo na wengi wanaogopa kuhusishwa katika kesi hiyo kwa kuwa bado
uchunguzi wake unaendelea.
“Napingana na hoja ya kusema sisi mastaa
ni wanafiki, binafsi ninachokiogopa mimi na wenzangu ni majumba mabovu
ambayo yanaendelea kubomoka (kuingizwa kwenye tuhuma) kila siku
kuhusiana na kesi ya Lulu, ndiyo maana wengi wanaogopa kwenda Segerea,”
alisema kiongozi huyo.
Lulu ambaye anatuhumiwa kuhusika na kifo cha Kanumba, ameshapandishwa kizimbani mara moja na atarejea tena Aprili 23, mwaka huu.
Kanumba
alifariki dunia usiku wa kuamkia Aprili 7, mwaka huu, nyumbani kwake
Sinza Vatican, Dar na kuzikwa Aprili 10 katika makaburi ya Kinondoni.
No comments:
Post a Comment
wadau unakaribishiwa kutoa comment ilimradi ziwe za kujenga na kuelimisha pia