Saturday, June 23, 2012

JACQUE PATRICK ALA BATA WAKATI ABDULLATIF FUNDIKIRA AKIWA NDANI




SIKU chache baada ya mumewe kuswekwa rumande kwa tuhuma za kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya, ‘model’ maarufu Bongo, Jacqueline Patrick amenaswa akila bata bila ya kuwa na wasiwasi ndani ya Ukumbi wa Nyumbani Lounge, jijini Dar, Ijumaa Wikienda linakujuza.
Jack aliyekuwa ametinga nguo nyeusi Na njano akiwa na kampani kubwa ya watu wake wa karibu, alikuwa akijiachia kama vile mtu asiyekuwa na uchungu na tukio la mumewe kuswekwa rumande.
Baada ya kumuona akiwa katika hali hiyo, mwandishi wetu alimzukia mnyange huyo na kumuuliza kulikoni ‘anaspendi’ wakati mumewe yupo nyuma ya nondo, akajibu kuwa hana jinsi, bora ajiliwaze na kupunguza mawazo kutokana na maumivu aliyonayo juu ya tukio hilo.
“Mpaka sasa mume wangu hajatoka selo, jambo ambalo linaniumiza lakini nakosa la kufanya ikizingatiwa kuwa ndoa yetu bado ni changa, kwani ndiyo kwanza tulikuwa tukijipanga kimaisha lakini matatizo yameanza kutuandama,” alisema.
Jack alisema kuwa anaona ni heri ajirushe na kujichanganya na watu kuliko kukaa nyumbani peke yake, kwani akiwa huko huwa anaumia mara mbili kutokana na kutawaliwa na mawazo mengi yanayotokana na upweke.
“Hapa nimekuja kwa ajili ya kupunguza mawazo tu, naumia sana kwani mume wangu ninampenda na nitazidi kumpenda milele kama nilivyoapa wakati tulipofunga ndoa, sitamuacha kwenye shida na raha, naendelea kumuomba Mungu ili atoke mapema,” alisema Jack.
TUJIKUMBUSHE
Hivi karibuni, mume wa Jack, Abdullatif Fundikira alikamatwa akiwa amejificha darini baada ya Jeshi la Polisi kuvamia nyumbani kwa wanandoa hao pande za Mbezi Beach jijini Dar.
Abdullatif anashikiliwa na polisi baada ya kuhusishwa na biashara ya madawa ya kulevya na mwanamke mmoja aliyekamatwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar.
IMERIPOTI GAZETI LA UDAKU...

1 comment:

  1. Hakuna mtu ana muda na upumbavu, yeye azidi kujiuza tu

    ReplyDelete

wadau unakaribishiwa kutoa comment ilimradi ziwe za kujenga na kuelimisha pia