CHADEMA WATEMBELEA IKULU KUJADILI MCHAKATO WA KATIBA......
.Chama Cha National Convention for Construction and Reform-Mageuzi (NCCR-Mageuzi) kimempongeza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kusimamia suala la Katiba vizuri na kwa umakini mkubwa. Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Bwana James Mbatia ametoa pongezi hizo leo jioni alipofika Ikulu, akiongoza ujumbe wa viongozi wenzake sita(6), kuja kujadili suala la Katiba Mpya ya Tanzania. "Tunakupongeza kwa kusimammia suala la Katiba vizuri, ni suala zito ambalo litatupa uhai vizazi na vizazi vijavyo". Amesema kama utangulizi wa ujio wao Ikulu. "Upinzani sio uadui, tunahitaji kufanya marekebisho ya Katiba kwa amani na hoja bila kuvuruga amani yetu” Bwana Mbatia amesema na kuongeza kuwa “suala la Katiba linahitaji ushirikiano wa pamoja kwa nia njema, kwani taifa hili ni letu sote" ameeleza. Akiwakilisha hoja ya NCCR-Mageuzi kwa Rais Kikwete, Mkuu wa Idara ya Sheria wa NCCR-Mageuzi Dkt. Senkondo Mvungi amesema, NCCR - Mageuzi inatambua ukubwa wa jambo hili la wa Tanzania kupata Katiba. "Ni jambo kubwa sana, wewe ndiyo Rais wa kwanza kutengeneza sheria ya kupata katiba mpya na kuanzisha Mchakato wa kupata Katiba Mpya. Kikao cha leo cha Rais na viongozi wa NCCR-Mageuzi ni mwendelezo wa jitihada za Rais Kikwete, kusikiliza, kuchukua maoni na mawazo ya wadau mbalimbali kutoka vyama vya siasa, asasi za kijamii na makundi mbalimbali katika kuelekea mchakato wa kupata Katiba Mpya ya hapa nchiniTanzania.
No comments:
Post a Comment
wadau unakaribishiwa kutoa comment ilimradi ziwe za kujenga na kuelimisha pia