Ama kweli kume kucha sana Dar hasa ukizingatia kundi la minenguo ya pwani lijulikanalo kama Kanga moja Moko Moko lenye msemo mpya lakini maarufu usemao "laki si Pesa, Milioni Mgogoro" Mitaa ya juzi kati walitia fora ndani ya ukumbi mpya wa DAR LIVE hapo mitaa ya kwetu Mbagalaaa!!
Kundi hili linalosadikiwa kuleta tafrani hasa kwa kuwapagawisha kaka Zetu wakiwemo waume za watu, waliporomosha burudani ya kukata mauno kwa kwenda mbele kuthibitisha ule msemo wao mwingine unaowaambia washabiki waone jinsi kanga inavyo vyaliwa, Ulileta tafraani kubwa pale kundi hilo lilipo paramia jukwaa la kisasa na kuwapagawisha mashabiki wao kikweli kweli.
Burudani yao kanga Moko ndembe ndembe ilisindikizwa na Burudani kutoka Extra bongo na Mashujaa Band bila ya kumsau Jike la simba bibie Isha Mashauzi, ili tia fora sana kwa watu wa Mbagala na kuacha gumzo kuu ndani ya jiji hili la Sadik.
Ingawa kundi hili linaongoza sana katika miondo ya yonga hapa jijini na lilikua na wapinzani wake kama Kitu-K na kitu -T sasa hivi limepata wapinzani wakubwa sana wakata nyonga wenzao kutoka mji ule wa waja leo waondoka leo yaani Tanga, kundi ambalo linajulikana kama Baikoko. Kundi hili lilileta tafrani ya aina yake pale lilipo kutanishwa na kundi hili la Kanga Moko.
Hapa sasa sijui ndio mieleka ama ndio staili.
Katika hali hiyo hiyo Muimbaji kutoka visiwa vinavyosifika kwa kuzalisha zao la karafuu hapa nchi yaani A.T. alijitokeza za na wanenguaji wake nao wakiwa na staili hizo hizo ambazo wengi tuliwaona katika video za nyimbo zake alizoshirikiana na kikundi cha offside Trick nacho cha huko huko visiwani, walionyesha umahiri mkubwa wa kupambana na kikundi hiki cha kanga moko hivyo kuleta upinzani mkubwa na burudani kwa washabiki wao ambao wengi ni wakina kaka.
Mmoja kati ya wanenguaji wa kundi la kanga moko
Tukiachana na burudani inayoletwa na kundi hili pia kume kuwa na tuhuma kuu kuhusuana na wakina dada hawa (wanenguaji) kujihusisha na waume za watu. Ingawa tuhuma hizo blog hii haijaweza kuthibitisha lakini inatoa ushauri wa bure kwa wana kundi hili na wengine kama hawa kwamba walete burudani lakini wasijihusishe na tabia za kuchukua waume za watu, kisa? wamewafwata wenyewe hivyo watunze maadili na kuheshimu kazi yao haswa ukizingatia ajira zenyewe ni za kutafuta sana.
No comments:
Post a Comment
wadau unakaribishiwa kutoa comment ilimradi ziwe za kujenga na kuelimisha pia