Thursday, February 2, 2012

Eti kuna Bifu kati ya Steven Kanumba na' Ray' Kigosi?

Katika Pita pita zangu Kitaa nikasikia watu wanasema eti Steven Kanumba a.k.a Kanumba the great na Vicent Kigosi a.k.a Ray haziungi kabisa. Ilinibidi nishangae yaani hawa maswaiba wa kufa na kuzikana kulikoni tena ikanibidi nizame sehemu sehemu ili niweze kuupata huu ukweli.


Sasa nikiwa natafuta vyanzo ama chanzo cha hawa maswahiba kutemana, nikaja kuupata ukweli kwamba lipo bifu la chini kwa chini ingawa si rahisi kuli baini bifu hilo kwasababu hawa wote ni wazoefu wa mambo yanayoenda mtandaoni hivyo kila mmoja huu chuna na kumpiga mwenzake kijembe cha chini kwa chini.

Lakini imesikika kwamba chanzo cha ugomvi baina yao ni maneno tu yalizuka yaliko zuka na yakawafikia alafu pwaaa!! Urafiki ukafa. Inasemekana ugomvi wao unawafanya wasiongee na ushahidi mzuri ni juzi kati katika msiba wa mzee Kipara ambapo kila mmoja hakuwa na muda na mwezie ingawa walikua msibani wote na kwenye mazishi walishiriki lakini hakukua na uswahiba wowote kati yao kama vile tuonavyo kwenye filamu walizocheza pamoja.


kati ya maneno maneno yalioko kitaa kuhusina nao ni kwamba inasemekana kwamba Kanumba ana tengeneza pesa zaidi kuliko Ray na kwamba yeye anapiga mzigo zaidi katika kuwakonga nyoyo za washabiki kwa umahiri wa kuigiza hivyo kumfanya Ray awe 'Second best'. Maneno haya yalipomfikia Ray, ingawa hayakutoka kwa Kanumba direct, yeye alijibu kwamba hawezi kuuza sura tu kwenye runinga nje ya fani ya uigizaji kwa manufaa ya kuuza sura huku ukipewa malipo madogo wakati akitengeneza muvi moja anapata mamilioni, ingawa alisema kwamba hamlengi mtu yeyote kwa kutamka maneno hayo lakini ni dhahiri alikua ana mlenga swahiba wake maana yeye ndio ana dili la kutangaza na kampuni iliyoingia ubia na TBC  katika kukamua ving'amuzi yaani 'Startimes'.

                            Mkoko wa Ray Kigosi Land Cruiser V8

Lakini hasa ni dhahiri kabisa chanzo cha ugomvi huo ni maneno tu yaliyo wafikia wahusika kuhusiana na mikoko ya nguvu wanayo ikokota kitaani ambapo Ray alisema mkoko wake aina ya V8 aliununua kwa bei ya milioni 78 wakati kiukweli inasemekana aliuvua kwa mtu kwa kiasi cha Milioni 35. Wakati mwenzake Kanumba ameuvuta mkoko wake aina ya Lexus kwa bei ya milioni 78 na akaitoa 'kesh maneee' kama vijana wa mtaani wanavyavyosema. 

                     Mkoko wa Kanumba The Great 'Lexus'

Mwisho wa siku Blog hii ilibaini bifu kati yao lakini sio kwamba ndio wanachukiana kupitiliza ila tu ni kwamba upepo mbaya umepita hapo kati kati na hali ya hewa imechafuka kutokana na wapambe nuksi, lakini wengi tunatarajia kwamba watapana na kutupa vionjo vizuri katika tasnia inayokua upesi sana hapa inchini.

3 comments:

  1. Doooh hii kali mbona mimi so sikujua haya mambo, alafu kweli kujulikana na umaaarufu huleta magomvi

    ReplyDelete
  2. Kanumba will forever be 'THE GREAT' and the best. And Ray will always be second best. Even when Steven Kanumba is no more.

    ReplyDelete
  3. ya thats is very true Kanumba and was the best and har dworking
    hope will meet him in heaven when the triumpet of the Lord sounds

    ReplyDelete

wadau unakaribishiwa kutoa comment ilimradi ziwe za kujenga na kuelimisha pia