Thursday, February 2, 2012

Aunty Asia kuvuma tena na Onyesho la Lady In Red Reloaded 2012

                                         
Aunty Asia Idarous anatarajia kuvumisha tena lile onyesho lake ka nguvu hapo ijumaa ya tarehe 10 mwezi huu ndani ya hoteli ya Serena (Zamani Movenpick). Katika Onyesho hilo linaloletwa kwa udhamini mkubwa wa bia ya Redds.

Akizungumza na waandishi ndani ya ukumbi wa Nyumbani pale maeneo ya Best Bite (Kwa Jaydee) Aunty Asia alisema kwamba katika onyesho hili ameshirikiana na Kikale Youth center ili kusaidia kupambana na vita dhidi ya madawa ya kulevya. Katibu wa Kikale youth Center Bw. Maulid Mlawa alisema kwamba Kikale ni asasi isiyo ya kiserikali yaani NGO inayojihusisha na vijana katika kuwasaidia kupambana na madawa ya kulevya aidha kwa ushauri/ nasaha na kutoa misaada katika kufanya vijana walioathirika na madawa hayo kuweza kurudia hali yao ya zamani.



Bwana Mlawa alisema amejisikia fahari kubwa kwa asasi yake kushirikiana na Fabak Fashion chini ya udhamini wa REDDS katika kusaidia vijana kwa kupitia onyesho hili, na akizungumza pia meneja wa kinywaji hicho Victoria Kimaro amesema yeye kama mwakilishi wa kinywaji hicho ameona ni vyema kufadhili hili onyesho ingawa sio mara yao ya kwanza lakini waliona ni vyema wajiunge katika hili ili kuweza kuwasaidia vijana walio athirika kwa njia moja ama nyingine.



 Hafla hiyo iliyoandaliwa na kampuni  ya Fabak Fashions kwa kushirikiana na Kikale Youth Group itawahusisha wanamitindo zaidi ya 30 kutoka Tanzania ambapo wasanii tofauti akiwamo Chiddy Benz, watakuwepo siku hiyo kusindikiza onyesho hilo la mavazi.

No comments:

Post a Comment

wadau unakaribishiwa kutoa comment ilimradi ziwe za kujenga na kuelimisha pia