Kanumba the Great (kati kati) akiwa na Mama yake aitwaye Flora na Dotnata (kulia)
Hatimae yule Muigizaji wetu aliye shinda ya best male Actor ya Smiling faces Co. Amefunguka live jana kwenye kipindi cha take one kinacho endeshwa na Shost wangu kipenzi Zamaradi Mketema. Katika kinpindi hicho Kanumba aliamua kusema ukweli kuhusu maisha yake, alianza kwa kuonyesha mazingira anayo ishi kwake na Swahiba yake aliye mtambulisha kama PA yaani Personal Assistant wake. Hiyo ilikua sehemu ya kwanza ya kipindi hicho ambayo ilichukua takriban dakika chache kama tatu tu hivi kama ka intro ka namna flani.
AFUNGUKA KUHUSU MAISHA YAKE.
Katika kipengele kingine cha Kipindi hicho, Kanumba The Great alitema cheche kwa kusema "Unajua watu hawanijui vizuri, wakiniona hivi wana fikiri maisha yangu yalikua ya raha sana". "Ki ukweli maisha yangu ya utotoni hayakuwa ya furaha sana" alisema Steve huku akiwa kama vile anataka kulia lakini alijikaza. Alisema katika maisha yake alikua anamsumbua mama yake ajulikanae kama Flora kwamba alitaka kumjua babake.
Hiyo ndio iliyotokea katika hadithi yake na kwamba mama yake alimkubalia kwenda kwa baba yake maeneo ya huko kwa Shinyanga, lakini alisema zaidi huku akiwa si mwenye furaha yaani alikua anaonekana uncomfotable kuiongelea hadithi hii lakini alisema kwamba ni ukweli kwamba maisha yake upande wa baba yake hayakuwa mazuri kwani aliteswa sana na mke wa baba yake yaani mama yake wa kambo ambae hakumtaja jina.
kati ya mateso aliyo pata ni kama kisa cha yeye kumenye viazi alafu akaambia akawape Mbuzi wa mamake wa kambo, lakini kwasababu kule kwao kama nyumba za watanzania wengi huwa wana desturi ya kuchimba mashimo ya taka uani ambako mara nyingi kipindi cha usiku kunakua giza na hakuna mwangaza wa kutosha. hivyo yeye akaona ni vyema atupe hizo taka badala ya kuwapa mbuzi maana muda ulikua umepita. Baada ya Maza wake huyo kugundua alimlazimisha akaokote teka hizo zote shimoni na hiyo ilimuuma sana. Pamoja na haya yote Kanumba alisema utoto wake fimbo ilikua ndio mwongozo wake "yaani akitokea mtu asinipige ama kunitesa namwona ni mtu wa hali fulani tofauti kabisa" alisema.
Kanumba akiwa na watoto kitaa
ASEMA KUHUSU MAMA YAKE MZAZI.
Katika kusema ukweli alisema kwamba kati ya babake anayeitwa Charles Meshark na mamake yeye hata iweje mamake ndio ana mmaindi kabisa, kwasababu alikuwa upande wake siku zote. "Kuna wakati mama alikuja nichukua kwa baba, nadhani alisikia kwamba nateswa lakini mimi sikuwa na mwambia chochote wala kulala mika kitu...." alifunguka, "....alimpeleka baba ustawi wa jamii ili baba nae aweze kuchangia katika elimu yangu, na alivyorudi kipindi hiko nilikua darasa la sita nilikua na hamu sana kujua baba amesemaje maana nilikua nampenda sana baba yangu, lakini mama hakunijibu ila baadae nilikua nikasikia kwa marafiki zake walio kuja kumtembelea kwamba baba alilalamika kwamba mimi ni jambazi na nilikua namwibia mama yangu wa kambo jambo ambalo lilinisikitisha sana kwasababu sikuwahi kufanya hivyo". Hivyo kati ya wazazi wake yeye the great mama yake ndio best wake.
Akiwa kazini ndani ya 'Crazy Love'
KUHUSU KUOA
Katika swala la kuoa hiyo ni baada ya kumtambulisha mama yake, kulitokea kama kaubishani hivi kwasababu katika mambo ambayo yangempendeza mama yake ni kama angeoa na kumpatia wajukuu. Lakini hiyo kwa Kanumba alimwachia Mungu "Unajua mama mambo haya siyo ya kukurupuka tu, ni lazima mtu ujiopange kama unavyojua tena mke mwema anatoka kwa Mungu hivyo Mungu akipenda nitaoa mama".
Licha na haya yote Kanumba alisema kwamba anapenda sana watoto ndio maana sinema zake nyingi ana cheza na watoto, maana watoto ni changamoto maana huwezi kujua atakua nani akiwa mtu mzima. Kipindi kitaendelea wiki ijayo ambayo sehemu ya pili itarushwa kama kawaidia jumanne saa tatu usiku mpaka saa tatu na nusu, ni Take one na Zamaradi Mketema ndani ya Clouds Tv 'the peoples station'
No comments:
Post a Comment
wadau unakaribishiwa kutoa comment ilimradi ziwe za kujenga na kuelimisha pia