Saturday, February 11, 2012

WEMA APATA MKOKO MPYA

Kulikua na tetesi kwamba Wema Sepetu amehongwa mkoko aina ya Lexus ambao anatamba nao kila kona la jiji hili kwamba amehongwa na bwana wake aitwae Clamence. Habari katika vyanzo vingi vinasema kwamba baada ya kumfurahisha huyo jamaa wake na uzuri alionao ikampendeza huyo jamaa kumhonga gari ili eti asiingie katika vishawishi vya wanaume wasio kua na maana kama ma bwana zake waliopita.

Hayo yote yalikua hewani kila Wema alipopita na Mkoko wake kiasi kwamba ikabidi kazi ya ziada iingie kwa wadau ili waweze kuupata ukweli. Lakini tisa kumi ukweli sio kama tulivyosikia, uzushi umekua mwingi sana juu ya Wema kiasi kwamba ilibidi aseme mengi alipohojiwa na Salama Jabir katika kipindi chake kipya kiitwacho Mikasi juu ya jambo asi lolote kuhusu yeye. Sasa basi tukija katika mada yetu ni kwamba Wema alipewa Gari hilo lenye namba za usajili T 211 BXR, amenunuliwa na mama yake pamoja na ndugu wengine kufuatia kufurahishwa na uamuzi mgumu aliouchukua.

 Akizungumzia madai hayo, Wema alisema wanaoamini amehongwa gari hilo wanakosea kwani ukweli ni kwamba amenunuliwa na ndugu zake kama zawadi.
“Najua kila mmoja atakuwa na lake la kusema juu ya hili gari ninalotumia kwa sasa, ukweli ni kwamba nimenunuliwa na mama na ndugu zangu wengine baada ya kutoka kwenye kashikashi zito na Diamond.
“Na mimi zaidi ya kuwashukuru pia naahidi kutowaangusha na nitajitahidi kutowakosea kwa namna yoyote ile,” alisema Wema.
Blog hii inapenda kumpongeza Wema kwa kupata mkoko wa maana wenye thamani kubwa ikiwa kama kifuta jasho kutoka kwa wana ndugu wake kwa kuamua kufanya maamuzi magumu ya kuachana na Diamondz Platnumz.

BADO SAVEI YETU INAENDELEA KATI YA WEMA NA JOKATE ACHA COMMENTS ZAKO KWENYE POST HAPO CHINI.

No comments:

Post a Comment

wadau unakaribishiwa kutoa comment ilimradi ziwe za kujenga na kuelimisha pia