Saturday, March 3, 2012

Mastaa wampongeza Kanumba kumchana baba yake

KATIKA hali isiyotarajiwa na wengi, baadhi ya mastaa wa filamu Bongo wamempongeza mwenzao Steven Kanumba kwa kitendo cha kumchana baba yake.
Kanumba wiki iliyopita kupitia Kipindi cha Take One kinachorushwa hewani kupitia Clouds TV alimtolea uvivu ‘mshua’ wake, Mzee Charles Kusekwa akidai amechangia katika mateso aliyoyapata utotoni mwake.
Baada ya Kanumba kueleza hayo, baadhi ya watu wakiwemo wasanii wenzake walimshangaa na kueleza kuwa kitendo alichokifanya si cha kiungwana kwani mzazi ni mzazi tu, hata kama amekosea si sahihi kumdhalilisha.
Hata hivyo, wapo wasanii waliompongeza msanii huyo kwa uamuzi aliochukua wakidai ni njia sahihi ya kutoa machungu yake. Walichokisema wasanii hao nenda ukurasa wa 6.

No comments:

Post a Comment

wadau unakaribishiwa kutoa comment ilimradi ziwe za kujenga na kuelimisha pia