Saturday, March 3, 2012
MASKINI DOTNATA
STAA wa filamu Bongo aliye mjasiriamali na mlezi wa wasanii nchini, Husna Posh ‘Dotnata’ yupo kitandani akiugulia maumivu makali baada ya kufanyiwa upasuaji wa tumbo na kutolewa uvimbe (nyama) wenye uzito wa kilo mbili, imeelezwa.
kutoka kwa mtu wa karibu na msanii huyo ambaye ana sifa ya kusaidia wenzake, zinasema kwamba Dotnata amezidiwa sana kabla ya kulazwa na kupata matibabu.
ILIANZA KAMA UTANI...
Chanzo hicho kwa sharti la kuhifadhiwa jina lake, kilieleza kwamba, maradhi ya msanii huyo yalianza kumsumbua muda mrefu lakini alipuuzia akiamini ni ugonjwa wa kawaida tu.
“Ilianza kama utani, Dot (Dotnata) alikuwa akisikia maumivu na kumeza vidonge vya kawaida kisha maisha yanaendelea, kumbe alikuwa na uvimbe tumboni. Alipokwenda hospitali na kugundua hilo, alishangaa sana, lakini tayari tatizo lilikuwa limeshakuwa kubwa,” kilieleza chanzo hicho na kuongeza:
“Madaktari walisema, kama angewahi kidogo, angeweza kupata tiba tofauti na upasuaji, na kama angelazimika kufanyiwa, basi ingekuwa operesheni ya kawaida.
DOTNATA KITANDANI
“Ni kweli ndugu yangu, naumwa nipo kitandani, lakini nimesharuhusiwa, kwa sasa nipo nyumbani,” alisema kwa sauti ya taratibu sana akionekana kuugulia maumivu.
Akizungumza kwa tabu Dotnata alisema, alianza kupata maumivu ya tumbo muda mrefu kabla ya kuamua kwenda hospitalini kufanyiwa uchunguzi na kugundulika kuwa ana uvimbe.
“Mwanzoni nilipuuza, lakini maumivu yaliponizidia nikaamua kwenda (Hospitali ya) TIH (Tanzania Institute of Heart) na kufanyiwa vipimo vilivyoonesha kwamba nina uvimbe tumboni.
“Kwa kweli nilishtuka sana, lakini sikuwa na jinsi, ikanibidi nikubali kufanyiwa upasuaji kwa kuwa madaktari walisema ndiyo tiba pekee itakayonisaidia,” alisema na kuongeza:
“Ulikuwa uvimbe mkubwa, niliambiwa kwamba unafikia kilo mbili. Sikuamini kama kweli umetolewa tumboni mwangu, lakini kwa sasa namshukuru Mungu, ninaendelea vizuri. Kuna tofauti kubwa na ilivyokuwa mwanzoni.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
wadau unakaribishiwa kutoa comment ilimradi ziwe za kujenga na kuelimisha pia