Tuesday, May 17, 2011

WAZIRI NCHIMBI AKUTANA NA WASANII NDANI YA UKUMBI WA BASATA

WAONGELEA HAKI MILIKI NA MATATIZO MENGINE YANAYOWAKABILI.

                              Mh. Waziri Emmanuel Nchimbi



                      Wasanii waliohudhuria mkutano huo


Mheshimiwa waziri wa habari,vijana,utamaduni na michezo Dr Emmanuel Nchimbi leo ameongea na wasanii  na mashirikisho mbalimbali ya muziki wa Tanzania katika ukumbi wa BASATA ilala,
ktk maswala yaliyoongelewa ukumbini hapo kubwa kati ya hayo kubwa ni kuhusu HAKI MILIKI za wasanii hapa nchini waliongea wadau mbali mbali ila maada ilikuwa moja tu haki miliki,wasanii walisisitiza kukaziwa mkazo wa sheria inayosimamia haki miliki za wasanii na kuwepo adhabu kali kwa wale wezi wa kazi zao.mana kume kuwepo na tatizo moja polisi wala mahakamani hawajui adhabu gani anapewa mtu ambae atakutwa akiiba kazi za wasanii hawa.Mh. waziri alisikiliza hoja na badae kutoa kauli yake na kusema atayafanyia kazi haya yote waliiongea,nia nikupunguza najua atuwezi tukayamaliza haya matatizo yote ila tutajitahidi tuyapunguze angalau tukapiga atua alisema waziri Nchimbi.

No comments:

Post a Comment

wadau unakaribishiwa kutoa comment ilimradi ziwe za kujenga na kuelimisha pia