Monday, January 30, 2012

ETI DIAMOND ALIMFUMANIA WEMA MPAKA AKACHOKA




“Nikianza na suala la kumfumania kila kukicha akisaliti penzi letu kwa wanaume wengine, nilishamfumania Wema mpaka nikachoka.
“Listi ya wanaume wa Wema ni ndefu, lakini fumanizi kiboko ni lile nililomkuta kitandani kama alivyozaliwa akifanya …(kitu kibaya) na rafiki yangu…(staa wa filamu za Kibongo),” Diamond aliezea kwamba alimvuta pembeni akampa kisago, alimuomba msamaha yakaisha, lakini bado aliendelea na mabwana zake. "Kinachoniuma ni kitendo cha kunitangaza kuwa ameniacha wakati mimi ndiyo nimemuacha."


Kuhusu swala la kurudiana na Wema, Diamond alisema " ameshakuja nyumbani na watu kibao kuniomba msamaha na akalala kwangu, nilimwambia awaombe radhi mashabiki wangu kwa kunichafua ‘then’ sitakuwa na kinyongo moyoni mwangu, nitamsamehe kama binadamu lakini sijui kama tutashirikiana tena mambo ya chumbani".

Kuhusu Uhusiano wake na Jokate Mwegelo, Diamond alikana kwamba hakuwa na uhusiano wowote, " Namheshimu sana Jokate, sijui ningeanzia wapi kumtongoza. Aisee, asikwambie mtu, Wema alimchafua mtoto wa watu bila sababu yeyote na wivu wake wa kimapenzi. Hakuna kitu Jokate anachojuta kama kukubali kufanya video yangu kwani tukio moja tu, lilimharibia vibaya ‘future’ yake".


Kutokana na hali hiyo, mashabiki wengi wa Wema na Diamond wameshauri kwamba kuliko kuchafuana majina na kuharibiana kwenye mitandao tofauti, ni vyema Wema na Diamond wakutanishwe ili haya maswala yamalizike maana wengi hasa vyombo vya habari vinachukua nafasi hii kuuza habari zao kwa watu bila ya Wema na Diamond kufaidika chochote. Ni vyema maswala haya yakaisha baina yao kila mmoja akachukua hamsini zake.

1 comment:

  1. Kama mtu mzima ndaweza sema diamond, just leave wema she's fuckin bitch , she bitching around, remember she did sleep with your best friend ,there is one of the day she wanna sleep with your father too. Just becareful and stay away from her. Thanks amanidaniel32@yahoo.co.UK

    ReplyDelete

wadau unakaribishiwa kutoa comment ilimradi ziwe za kujenga na kuelimisha pia