Saturday, March 3, 2012

Shyrose Bhanji hoi nje ya nchi


MKUU wa Kitengo cha Mawasiliano cha Benki ya Makabwela (NMB), Shyrose Bhanji (pichani) hivi karibuni amewashitua watu baada ya kuposti picha kwenye ukurasa wake wa Facebook ikimuonesha amelazwa katika hospitali moja inayodaiwa iko nje ya nchi.
Picha hiyo ambayo pia inapatikana katika mitandao mingine bila kutaja kuwa ni hospitali gani na ipo nchi gani, inamuonesha mwanadada huyo akiwa hoi kitandani, hali iliyowafanya wadau kuhoji juu ya kinachomsumbua.
“Dah! Pole sana dada Shyrose, Mungu akujaalie upone haraka, tatizo nini? alihoji Jack huku mwingine aliyejitambulisha kwa jina la John akiandika: “Taarifa hizi zimenishitua sana, Watanzania tumuombee mpendwa wetu apone haraka ili arejee katika shughuli za ujenzi wa taifa.”
Kufuatia ‘comments’ hizo zipatazo 900 za wadau zilizokuwa zikimpa pole na nyingine kutaka kujua ugonjwa uliomlaza, Shyrose alilazimika kufunguka:
“Ni dehydration (upungufu wa maji mwilini) na fatigue (uchovu) but naendelea vizuri. Nimepatwa na homa kali sana na ninasikia baridi mpaka kwenye mifupa...ninajisikia vibaya sana na niko tu kitandani kitu ambacho
Aidha, siku chache baadaye Shyrose aliandika kuwa ametoka hospitalini na anaendelea vizuri.
“I have been discharged and I feel so much better than the last few days. I am happy to see that I am loved, thanks all very much... I will be back home soon…(Nimeruhusiwa na naendelea vizuri tofauti na siku chache zilizopita. Ninayo furaha kuona napendwa, nashukuru sana..nitarudi nyumbani siku si nyingi,” alisema Shyrose huku ikionekana kuwa kweli alilazwa nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment

wadau unakaribishiwa kutoa comment ilimradi ziwe za kujenga na kuelimisha pia