Saturday, March 3, 2012
Dakika za mwisho za Whitney Houston
Safari ya maisha ya marehemu Whitney Houston ‘Queen of Pop’, aliyeaga dunia baada ya kuzidiwa na dozi ya dawa zinazotajwa kuwa ni za kulevya, ilifikia mwisho hapa duniani baada ya mwili wake kuzikwa katika makaburi ya New Hope Baptist Church, Newark, New Jersey, mahali alikozaliwa na kuanza kuonesha kipaji chake.
Mengi yamezungumzwa kuhusiana na kifo chake, lakini simulizi inayowatia simanzi wengi ni ile inayohusu saa za mwisho za uhai wake kabla ya kuaga dunia ambapo mtu wake wa karibu anayetajwa kuwa alikuwa mpenzi wake mpaka anaaga dunia, William Ray Norwood Jr. ‘Ray J’ anaelezea kwa masikitiko.
“Whitney alikuwa ni kama aliyekiona kifo chake kwani dakika za mwisho za uhai wake alikuwa anasema anatamani kwenda kuonana na Yesu na mara kwa mara alikuwa akinukuu vifungu vya Biblia vinavyoashiria mwisho wa maisha yake, jambo ambalo sikuwahi kumuona akilifanya tangu nianze kuwa naye.
“Kuna wakati alikuwa akizungumza mwenyewe maneno yasiyoeleweka na mpaka tukiwa naye kwenye Hoteli ya Beverly Hills sambamba na mwanaye, kuhudhuria sherehe ya Pre- Grammy, alikuwa haeleweki. Kuna wakati alikuwa analia mwenyewe, muda mwingine anacheka na muda mwingine alikuwa anamfokea kila mtu hadi kusababisha kupigana na mmoja wa watu pale ukumbini.
“Namuonea sana huruma binti yake, Bobbi Kristina Brown, 18, kwani alikuwa naye dakika chache kabla ya kifo chake, inasikitisha lakini mapenzi ya Mungu na yatimizwe, pumzika kwa amani Whitney,” alisema Ray J na kukaririwa na mtandao mmoja maarufu pande hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
wadau unakaribishiwa kutoa comment ilimradi ziwe za kujenga na kuelimisha pia