Saturday, March 3, 2012

SHILOLE: AVUNJIWA PUB YAKE

MCHEZA filamu za Kibongo ambaye ameanza kung’ara kwa kasi kupitia muziki, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ hivi karibuni aliangua kilio kama mtoto hadharani baada ya kukombwa kila kitu kwenye Pub yake iliyopo Kinondoni jijini Dar.
Akizungumza na Tollywood Newz huku uso wake ukiwa umetawaliwa na huzuni, Shilole alisema kuwa kabla ya tukio hilo kutokea alikuwa amenunua vitu vilivyokuwa vimepungua na kuvijaza lakini usiku wezi walifika na kuvunja kisha kuiba kreti tano za bia, tatu za soda pamoja na runinga.
“Jamani roho inaniuma sana kwani ndiyo kwanza naanza kujijenga halafu watu wanakuja kuniibia, mbona hawaendi kuiba kwa matajiri mpaka waje kunikwapulia kidogo ninachojitafutia?” alisema Shilole.
Staa huyo aliongeza kuwa pamoja na kukombwa vitu vyake hajakata tamaa, atafanya kila linalowezekana ili kukaa sawa.

No comments:

Post a Comment

wadau unakaribishiwa kutoa comment ilimradi ziwe za kujenga na kuelimisha pia