STAA wa muvi za Kibongo ambaye alipata maujiko kupitia ushiriki wake katika Shindano la Miss Kiswahili 2009 na kuuza nyago kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Rehema Fabian (pichani) anadaiwa kunywa sumu ya panya kisa kikiwa ni ishu za mapenzi.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Rehema alifanya tukio hilo nyumbani kwake Mbezi Beach, Dar es Salaam, asubuhi ya Ijumaa iliyopita, baada ya kuunganishwa kwenye fungu la mastaa wanaogombea penzi la pedeshee aliyetajwa kwa jina moja la Jacob.
“Rehema anaishi na Lilian (shosti wake), wakati ishu hiyo inatokea, Lilian alikuwa ametoka akamwacha peke yake ‘so’ nasikia alikwenda dukani akachukua sumu ya panya kwa kisingizio kuwa panya wamejaa ‘geto’ kwake,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
“Lilian aliporejea ndipo alipopiga makelele akiomba msaada kwa majirani hivyo Rehema akawahishwa Mwananyamala (hospitali), alipopata nafuu, usiku alichukuliwa na polisi na kwenda kufunguliwa shitaka la kutaka kujiua.”
Ilidaiwa kuwa baada ya kutoa maelezo polisi, Rehema ambaye afya yake ilikuwa haijatengemaa aliwekewa dhamana ambapo alirudishwa nyumbani na mashosti zake waliokuwa wakimsaidia.
Alipotafutwa na Ijumaa Wikienda, Rehema alidai hawezi kuzungumza kwani hali yake ilikuwa mbaya.
No comments:
Post a Comment
wadau unakaribishiwa kutoa comment ilimradi ziwe za kujenga na kuelimisha pia