Friday, January 27, 2012

IRENE UWOYA NA JANETH WANASWA LIVE MAISHA CLUB

                                                           
                                                        IRENE UWOYA


                                                       IRENE UWOYA

Irene Uwoya, alinaswa akiwa na Janeth Mathias ambaye aliyewahi kumtuhumu kuwa ndiye anayemharibia kwa mume wake, Hamad Ndikumana.
 marafiki zao wakaribu aliwashuhudia wawili hao wakiwa pamoja, wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa New Maisha Club, Masaki Dar, ambapo kulikuwa na event ya utoaji tuzo za heshima kwa wasanii wa sanaa hiyo iliyopewa jina la Mini- ZIFF Red Carpet.
Hafla hiyo iliandaliwa na Shirikisho la Filamu Zanzibar (ZIFF) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa filamu nchini ambapo wasanii kadhaa walitunukiwa tuzo hizo.
 I rine alipoulizwa akasema: “Usikonde ni mambo madogo, tumeshamalizana.”
Alipotakiwa kueleza namna walivyoyamaliza, hakutoa ushirikiano zaidi ya kusisitiza ni mambo yaliyopita na sasa ni marafiki kama zamani.
“Huyu ni shoga yangu, siku zote wagombanao ndiyo wapatanao. Sasa hivi tupo poa... usiwe na wasiwasi,” alisema na kuangusha kicheko kingine kabla ya kumtupia jicho shosti wake huyo.
Wasanii waliotunukiwa tuzo hizo ni pamoja na Jacob Steven ‘JB’, Thecla Mjata, Steven Kanumba na Vincent Kigosi ‘Ray’.
Wengine ni Juma Salum, Rose Ndauka na Issa Mussa ‘Cloud’.
Ray hakuwepo ukumbini hapo, hivyo swahiba wake ambaye inadaiwa wana bifu la chini kwa chini, Kanumba alimchukulia.

No comments:

Post a Comment

wadau unakaribishiwa kutoa comment ilimradi ziwe za kujenga na kuelimisha pia